Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amesema kamati ya uokozi imetengenezwa japo kiwango chake cha kuungwa mkono hakijulikani, BBC imeripoti.
Maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura wameripotiwa kuwa wanasherehekea kwa sasa.
Rais Nkurunziza kwa sasa yupo hapa nchini Tanzania.
Akaunti ya Twitter ya ikulu imesema mapinduzi hayo ya kijeshi yameshindwa.
Nkurunziza amekuwa akikutana na viongozi wengine wa Afrika Mashariki kujadili mgogoro huo. Msaidizi wake amekanusha kufanyika kwa mapinduzi hayo
0 comments:
Post a Comment