\ |
Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa
‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye
amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu
aliyeibuka na tuzo mbili.
D’Jaro alikuwa akishindana na Millard
Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia
kipengele cha blog inayopendwa.
“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.
“Lakini inakushtua kwa njia nzuri kwamba
kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa ufanyie kazi zaidi. Lakini pia
kura zinamata, inachangia sehemu zote, inawezakana ubora wa kipindi na
kura pia.
Lakini all in all mimi nampongeza sana
D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto pia, inatupa
nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya kazi kwenye
biashara yetu vizuri.”
Hii ni orodha kamili ya washindi
Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM
Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi – EATV
Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com
Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz
0 comments:
Post a Comment