Baba aua Binti yake, Amzika Nyumbani Kwake

JESHI la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake na kumyonga kwa kutumia kanga.

Akizungumzia tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na kumzika.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.

Alisema baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga shingoni.

Kwa taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo, maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,” alisema Mwaibambe
Share on Google Plus

About Bofya Tube

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment